MUSSA MUDDE ATEMWA SIMBA

MUSSA MUDDE ATEMWA SIMBA, 

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2012/07/Mussa-Mudde-vies-for-the-ball-with-Wamdale-Baker-of-Express.jpg
SIMBA SC imeendelea na harakati za kuimarisha kikosi chake na sasa inafikiria kuvunja mkataba na kiungo Mganda, Mussa Mudde wakati leo wachezaji wawili wengine wa kigeni beki, kutoka Tusker ya Kenya na mshambuliaji kutoka Ivory Coast wanatarajiwa kuwasili kujiunga na timu hiyo.
Lakini pia Simba inataka kuleta wachezaji wawili wengine kutoka Mali, ili iangalie wawili kati ya hao wanne kupata wakali zaidi wa kuunda kikosi cha kutisha msimu ujao.
Baada ya kugundua kikosini kuna viungo wengi, Simba inapunguza kiungo mwingine wa kigeni na kuongeza beki mmoja na mshambuliaji mmoja.
Tayari Simba imeacha kiungo mmoja wa kigeni, Kanu Mbivayanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kusajili beki Paschal Ochieng kutoka AFC Leopard ya Kenya na mshambuliaji Daniel Akuffo kutoka Hearst Of Oak ya Ghana, ambaye pia raia wa Ivory Coast.
Habari kutoka Arusha, ambako Simba imeweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu, zimesema kwamba katika siku ya kwanza ya mazoezi yao na kikosi hicho leo, wachezaji wote hao wawili wameonyesha viwango vya hali ya juu.
Imeelezwa kwamba, mshambuliaji Akuffo ni hatari mno na kwa haraka haraka hakuna wa kumfananisha naye kati ya washambuliaji wote waliopo Tanzania kwa sasa.
Anasifiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kasi, nguvu, ufundi na mbinu za kimchezo- maana yake Wekundu wa Msimbazi wamelamba dume. Kama wachezaji wapya wanaotua leo watamridhisha kocha Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick, Simba itamtema Mudde na kubaki na idadi ya wachezaji wa kigeni watano kama inavyoelekeza kanuni ya usajili ya Ligi Kuu kuhusu wachezaji wa kigeni.
Wachezaji wengine wa kigeni kwenye kikosi cha Simba SC ni washambuliaji Mganda Emmanuel Okwi na Mzambia Felix Sunzu.
Chanzo:- Bin Zubeiry

Post a Comment

Previous Post Next Post