MUSSA MUDDE ATEMWA SIMBA,
SIMBA SC imeendelea na harakati za kuimarisha kikosi chake
na sasa inafikiria kuvunja mkataba na kiungo Mganda, Mussa Mudde wakati leo
wachezaji wawili wengine wa kigeni beki, kutoka Tusker ya Kenya na mshambuliaji
kutoka Ivory Coast wanatarajiwa kuwasili kujiunga na timu hiyo.
Lakini pia Simba inataka kuleta wachezaji wawili wengine kutoka Mali, ili iangalie wawili kati ya hao wanne kupata wakali zaidi wa kuunda kikosi cha kutisha msimu ujao.
Lakini pia Simba inataka kuleta wachezaji wawili wengine kutoka Mali, ili iangalie wawili kati ya hao wanne kupata wakali zaidi wa kuunda kikosi cha kutisha msimu ujao.
Baada ya kugundua kikosini kuna viungo wengi, Simba
inapunguza kiungo mwingine wa kigeni na kuongeza beki mmoja na mshambuliaji
mmoja.
Tayari Simba imeacha kiungo mmoja wa kigeni, Kanu Mbivayanga
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kusajili beki Paschal Ochieng
kutoka AFC Leopard ya Kenya na mshambuliaji Daniel Akuffo kutoka Hearst Of Oak
ya Ghana, ambaye pia raia wa Ivory Coast.
Habari kutoka Arusha, ambako Simba imeweka kambi kujiandaa
na msimu mpya wa Ligi Kuu, zimesema kwamba katika siku ya kwanza ya mazoezi yao
na kikosi hicho leo, wachezaji wote hao wawili wameonyesha viwango vya hali ya
juu.
Imeelezwa kwamba, mshambuliaji Akuffo ni hatari mno na kwa
haraka haraka hakuna wa kumfananisha naye kati ya washambuliaji wote waliopo
Tanzania kwa sasa.
Anasifiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kasi,
nguvu, ufundi na mbinu za kimchezo- maana yake Wekundu wa Msimbazi wamelamba
dume. Kama wachezaji wapya wanaotua leo watamridhisha kocha Mserbia, Profesa
Milovan Cirkovick, Simba itamtema Mudde na kubaki na idadi ya wachezaji wa
kigeni watano kama inavyoelekeza kanuni ya usajili ya Ligi Kuu kuhusu wachezaji
wa kigeni.
Wachezaji wengine wa kigeni kwenye kikosi cha Simba SC ni
washambuliaji Mganda Emmanuel Okwi na Mzambia Felix Sunzu.
Chanzo:- Bin Zubeiry
Chanzo:- Bin Zubeiry
إرسال تعليق