MWANZO HADI MWISHO MAPOKEZI YA TWITE(PAMOJA NA JEZI YA RAGE)
Beki wa
kimataifa wa Yanga Mbuyu Twite akionesha jezi namba 4 aliyovikwa na
mashabiki wa Yanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege leo.
Jezi hiyo ambayo imeandikwa 'RAGE' ni jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail
Aden Rage inanokana ni kijembe kwa mahasimu hao wa Yanga ambao awali
walitangaza kumsajili kwa dau la dola 30,000 kabla ya Yanga kumpandishia
hadi dola 50,000.
Habari/Picha na:- Sports Lady(dinaismail.blogspot.com)
Hapa Twite akivishwa jezi hiyo yenye jina la Rage na mwanachama maarufu wa Yanga
Twite
akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema amekuja kufanya kazi
na hajali yote yaliyosemwa juu yake kujisajili timu mbili
Hapa Twite akiingia kupitia mlango wa watu mashuhuri (VIP) uwanjani hapo akiambatana na baadhi ya viongozi wa Yanga
Watu TWITE TWITE TWITEEEEEEEEEE
Kulikuwa na mbwembwe za kila aina na uwan ja ulifurika kwa rangi zxa njano na kijani
Matarumbeta , mdundiko vilikuwepo yote ni katika furaha ya ujio wa Twite
Kwa
mapenzi na timu yao hawakujali kama ni muda wa kazi, jua, mvua wala
kupoteza muda ,kwao ilikuwa ni full shangwe na hatimaye FILAMU Ya TWITE
ILIISHA.
إرسال تعليق