STAA
wa filamu na muziki wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ anadaiwa
kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kupenda uhusiano wa kimalavidavi na
vijana wadogo a.k.a Serengeti boys anaowazidi umri.
Chanzo kimedokezwa kuwa mwanadada huyo alikuwa akifanya siri lakini sasa imevuja kwamba amekuwa akibanjuka
na damu changa mfano ukitolewa kwa wasanii wenye umri mdogo ambao
aliwahi kujilainisha kwao kwa kuwahonga visenti na kuwapa gari lake
watembelee ‘tauni’.
Baada ya kuzitia habari hizo , http://freebongo.blogspot.com/ ilimnyatia Shilole na kumuuliza kama analolote la kusema, ndipo akatanua kinywa:
“Ninavyojua mapenzi hayachagui umri mkubwa wala mdogo, nawashangaa hao wanaosema hivyo, sasa wanataka niwe na wazee? Mimi ni kijana, lazima niwe na uhusiano na vijana wenzangu.”
إرسال تعليق