ULAYA LEO:- MAGAZETI, SONG, KAKA, NDANI

KAKA KUTUA MANCHESTER UNITED

Kaka
Kiungo wa kimataifa wa Brazil, mwenye umri wa miaka 30, Kaka amepewa ofa ya kwenda kucheza kwa mkopo wa muda mrefu Manchester United, wakati Real Madrid ikijiandaa kumpokea Luka Modric.
 

WENGER AMUUZA PAUNI MILIONI 15 SONG


Alex SongArsene Wenger ametaka pauni Milioni 15 kumuuza Alex Song kwenda Barcelona, baada ya kiungo huyo aliyezaliwa miaka 24 iliyopita kuonyesha wazi anataka kuhamia Camp Nou.
Habari kamili: Daily Mail

Daniel Agger, mwenye umri wa miaka 27, yu tayari kusaini mkataba mpya na Liverpool na 'kuitolea mbavuni' Manchester City - licha ya kulimwa kadi nyekundu katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya West Brom.
Habari kamili: Daily Mirror
 
 
Manchester City imejiunga kwenye mbio moja na Chelsea za kuwania saini ya mshambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic aliyezaliwa miaka 22 iliyopita.
Habari kamili: The Metro
 
 
 

Post a Comment

أحدث أقدم