Mohammad Saaili Shibin akipelekwa kuanza kifungo |
Raia mmoja wa Somali ambaye alikuwa ajenti wakati wa
mzungumzo kuhusu kuachiliwa kwa mateka wa Marekani amefungwa miaka 12
nchini marekani.
Mohammad Saaili Shibin alipatikana na hatia
mwezi wa April kwa makosa ya Uharamia, utekaji nyara wakati wa mshua ya
kifahari ya SV Quest ilipotekwa nyara na maharamia wa Kisomali karibu na
Oman.
Mkuu wa mashitaka aliambia mahakama kuwa Shibin alipokea kiasi cha dola $30,000 (£18,475) kwa kazi yake ya uajenti wa maharamia.
Mateka wote wa Kimarekani waliokuwa ndani ya chombo hicho walipigwa risasi na kuuwawa.
Katika mahakama ya Norfolk, mjini Virginia, Jaji
Robert Doumar aliamuru Shibin atumike vifungo 10 vya maisha gerezani ,
lakini vifungo hivyo viende sambamba.
Wakala huyo wa Maharamia pia aliamriwa alipe faini ya dola milioni $5.4m ili kufidia waliopata hasara kutokana na mkasa huo.
"Mohammad Shibin ni mshiriki mkuu katika kisa
hiki kibaya zaidi cha uharamia ambacho kimewahi kushuhudiwa katika enzi
hii" alisema mkuu wa mshitaka Neil MacBride.
Mahakama hiyo iliambiwa jinsi Shibin alitafiti
katika mtandao kujua undani wa mateka hao wa kimarekani ili kukadiria
kima cha pesa wanazoweza kulipa kama kikombozi.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo pia mahakama
ilisikia jinsi Shabin alifanya juhudi za kwatafuta jamii ya mateka hao
ili kuwaambia pesa maharamia wanazodai kama kikombozi.
Shibin alikamatwa na shirika la kijasusi la
Marekani FBI wakishirikiana na wanajeshi wa Marekani ndani ya Somalia
mwezi Aprili,2011.
Wakili wake amesema watakata rufaa.
Chanzo:- BBC Swahili
إرسال تعليق