![Ramani ya Kenya](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/06/29/120629123452_kenya_map_dadaab_304x171_bbc_nocredit.jpg)
Mauaji hayo yilitokea wakati watu wenye silaha
kutoka jamii ya Pokomo waliposhambulia kijiji kimoja katika eneo la
Reketa huku wakiteketeza makaazi ya watu.
Naibu
kamanda wa polisi mjini Mombasa, Joseph Kitur, amethibitisha kuwa watu
48 waliuawa, 31 kati yao ni wanawake, watoto 11 na wanaume sita.
Ng'ombe wapatao 60 vile vile walikatakatwa na wavamizi hao.
Kitur amesema shambulio hilo ni la kushangaza
kwa kuwa watu 34 waliuawa kwa kukatakatwa mapanga, wengine 14 nao
waliteketea hadi kufa katika nyumba zao.
Amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa shambulio hilo lilifanywa na watu kutoka jamii ya Pokomo.
Tangu mwezi uliopita, jamii hizo mbili zimekuwa
zikipigana kuhusu umiliki wa ardhi inayotumiwa kama eneo la malisho ya
mifugo, lakini shambulio hilo la Jumatano ndilo baya zaidi kuwahi
kutokea katika historia yao.
Ripoti zinasema polisi wanawasaka wale waliofanya mashambulio hayo.
Kuna taarifa kuwa watu kadhaa wamekamatwa na polisi lakini mkuu huyo wa polisi hakuthibitisha ripoti hizo.
Idara ya polisi imesema uhasama kati ya jamii
hizo mbili umekuwa ukitokota kwa muda, lakini hapakuwa na ishara ya
fununu yoyote kuwa shambulio hilo la Jumatano lingetokea.
Mwaka wa 2001, takriban watu 130, waliuawa kwenye mapigano katika maeneo ya mipakani kati ya jamii hizo mbili.
Mbunge wa Eneo hilo, Danson Mungatana, amesema
shambulio hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mashambulio mengine
yaliyofanywa na jamii ya Orma ambapo mamia ya mifugo iliibwa.
Chanzo:- BBC Swahili
إرسال تعليق