WELBECK ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MINNE - MAN U

New deal: Danny Welbeck signs his contract with Manchester United chief executive David Gill
Mshambuliaji matata wa Manchester United Danny Welbeck amesaini mkataba mpya wa miaka minne, na sasa atasalia katika klabu hiyo hadi mwaka wa 2016.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, alifunga mabao kumi na saba kutokana na mechi 64 alizoichezea Manchester United na vile vile alishirikishwa katika kikosi cha England kilichoshiriki katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika.
'' kile ambacho nimekuwa nikitaka kufanya ni kuichezea Manchester United, ni klabu ambayo nimeiunga mkono maishani mwangu'' alisema Welbeck.
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema, Welbeck amekuwa mmoja wao tangu alipokuwa na umri wa miaka minane na katika miaka ya hivi karibu, mchezaji huyo amebobea.
Welbeck alicheza mechi yake ya kwanza na Manchester United Septemba mwaka wa 2009 dhidi ya Middlesbrough.
Tangu wakati huo mchezaji huyo amekuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa lakini sasa anakabiliwa na upinzani mkali, hasa baada ya United kumsajili aliyekuwa naodha wa Arsenal Robin Van Persie.
Under threat: Welbeck faces competition for a starting place from new signing Robin van PersieKwa sasa Ferguson ana washambuliaji kadhaa katika kikosi chake na ni pamoja na Welbeck, Van Persie, Wayne Rooney, Javier Hernandez, Dimitar Berbatov na Federico Macheda.

Post a Comment

أحدث أقدم