Taifa Stars |
TIMU ya ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepangiwa kucheza na Uganda, The Cranes
katika raundi ya kwanza ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika Afrika Kusini mwaka 2014.
Kwa mujibu
wa ratiba iliyopangwa jana (Septemba 7 mwaka huu) makao makuu ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Cairo, Tanzania imeingia moja kwa moja
raundi ya kwanza ambapo itacheza na Uganda.
Mechi ya
kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kati ya Juni 21,22 na
23, 2013 wakati ya marudiano itakuwa Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini
Kampala kati ya Julai 5,6 na 7, 2013.
Nchi 38
zinashiriki katika mechi hizo za mchujo ambapo nyingine zitaanzia raundi ya
awali itakayochezwa kati ya Novemba 30 na Desemba 1 na 2 mwaka huu wakati mechi
za marudiano zitakuwa kati ya Desemba 14,15 na 16 mwaka huu.
Ratiba
imepangwa kwa makundi ya kanda ambapo jumla ya timu 16 ndizo zitakazocheza
fainali hizo nchini Afrika Kusini. Kanda hizo ni Kaskazini itakayopeleka timu
mbili katika fainali, Magharibi A (timu mbili), Magharibi B (timu tatu), Kati (timu
tatu), Kati Mashariki (timu tatu), Kusini (timu tatu akiwemo mwenyeji Afrika
Kusini).
Kwa upande
wa kanda ya Tanzania (Kati Mashariki), timu zinazoanzia raundi ya awali ni
Burundi, Eritrea, Ethiopia na Kenya.
Fainali za
Kwanza za CHAN zilifanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast ambapo Tanzania
ilishiriki huku Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ikiibuka bingwa. Fainali
za Pili zilichezwa mwaka 2011 nchini Sudan ambapo Tunisia ilitwaa ubingwa.
Fainali za Kwanza zilishirikisha timu nane kabla ya kuongezwa hadi 16 za sasa.
Post a Comment