NEWS: WAISLAMU WAANDAMANA HADI KWENYE OFISI ZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI


Maandamano hayo yakielekea katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa kundi kubwa la waumini wa dini ya kiislamu wameandamana hadi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, maeneo ya posta.
Haijafahamika mara moja maandamano hayo yanalenga nini lakini habari ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa maandamano hayo yanashinikiza kuachiwa huru kwa mwenzao anayeshikiliwa na jeshi la polisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post