![]() |
| Kazimoto |
Na Mahmoud Zubeiry
MWINYI
Kazimoto amepewa zawadi ya dola za Kimarekani 3,000, zaidi ya Sh.
Milioni 4.5 kwa kufunga bao la ushindi juzi dhidi ya Azam FC katika
mechi ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini fedha
hizo atagawana na wachezaji wenzake ‘kiungwana’.
Pamoja
na hayo, inasemekana, Mganda Emmanuel Okwi ndiye aliyevuna fedha nyingi
kutoka kwa wadau wa Simba, waliofurahishwa na bao lake tamu la
kusawazisha katika mechi hiyo, ambayo Simba ilitoka nyuma kwa mabao 2-0
na kushinda 3-2, bao lingine akifunga Mghana, Daniel Akuffo kwa
penalti.
Pamoja na zawadi hizo binafsi, Simba
imewapa wachezaji wake bonasi ya Sh. Milioni 15 wagawane kwa kutwaa
Ngao ya Jamii, wakiifunga Azam FC mabao 3-2 juzi Uwanja wa Taifa mjini
Dar es Salaam.
Habari kutoka ndani ya Simba, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata
zimesema kwamba, fedha watagawana wachezaji na benchi zima la ufundi la
klabu kwa ushujaa wao wa kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2
dhidi ya Azam FC jana.
Simba
SC, ilitwaa Ngao ya Jamii juzi, baada ya kuifunga Azam FC, mabao 3-2,
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar e s Salaam, shukrani kwake kiungo Mwinyi
Kazimoto Mwitula aliyefunga bao la ushindi dakika ya 78 kwa shuti kali
la mbali baada ya kumchungulia kipa wa Azam, Deo Munishi ‘Dida’
amekaaje.
Hadi
mapumziko, Azam walikuwa mbele kwa mabao 2-1, yaliyotiwa kimiani na
John Raphael Bocco ‘Adebayor’ na kipre Herman Tchetche, wakimtungua kipa
namba moja Tanzania, Juma Kaseja.
Bocco
alitangulia kufunga dakika ya tano ya mchezo huo, baada ya kupigiwa
kona fupi na Abdi Kassim ‘Babbi’, akatoa pasi kwa Abdulhalim Humud
ambaye alimrudishia mfungaji huyo akafumua shuti kali la chini likajaa
nyavuni pembezoni mwa lango kulia.
Bocco
ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Simba SC leo,
alimtoka Amir Maftah upande wa kulia wa Uwanja na kuingia ndani kabla ya
kutoa krosi fupi kwa Kipre aliyemtungua Kaseja na kuipatia Azam bao la
pili dakika ya 35.
Simba
ilipata bao lake la kwanza dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza, baada
ya kutimu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza, mfungaji Daniel Akuffo
kwa penalti, baada ya Said Mourad kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi
cha pili Simba walirudi na nguvu zaidi na kuamua kushambulia kwa mipira
ya pembeni, ikiwatumia Mrisho Ngassa na Emanuel Okwi ambao walikuwa
wakibadilishana reli.
Kwa
staili hiyo, haikushangaza Simba ilipotumia dakika 45 za mwisho kwa
kufunga mabao mawili yaliyowatoa nyuma kwa 2-1 na kuibuka kidedea kwa
ushindi wa 3-2.
Emanuel
Okwi alimchambua kama karanga Erasto Nyoni na kuingia ndani kabisa
akiwatoka mabeki wengine wa Azam, kabla ya kuujaza mpira nyavuni kwa
shuti kali na Kazimoto akamaliza kazi dakika ya 78.
Kwa
ujumla katika mchezo huo, Azam ilitawala kipindi cha kwanza na ilikosa
mabao mawili zaidi ya wazi kupitia kwa Himid Mao na Kipre, lakini
kipindi cha pili Simba walitawala mchezo na kama wangekuwa makini, nao
wangeweza kuvuna mabao zaidi.
Naibu
Waziri wa Kazi, Makongoro Mahanga alimkabidhi ngao Nahodha wa Simba,
Juma Kaseja baada ya mechi hiyo, ambaye alikwenda kushangilia na
wachezaji wenzake na mashabiki wa timu hiyo.
Hiyo inakuwa mara ya pili mfululizo Simba wanatwaa Ngao, baada ya mwaka jana pia kuibeba wakiifunga Yanga 2-0.
Aidha,
hiyo inakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa kihistoria nchini
na ya pili kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya
Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa
ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao
2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya
Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao
kihistoria.
Katika
mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi
Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka
jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga
Yanga mabao 2-0.
Ikumbukwe
mara ya mwisho Simba SC ilipokutana na Azam FC, katika Robo Fainali ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Julai mwaka huu,
Dar es Salaam, ilifungwa mabao 3-1, yote yakifungwa na Bocco na lile la
kufutia machozi kwa wekundu hao Msimbazi liliwekwa kimiani na kiraka
Shomari Kapombe.
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba kilikuwa; Juma
Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Paschal Ochieng/Juma
Nyosso dk 73, Shomary Kapombe, Ramadhan Chombo/Amri Kiemba dk69, Mrisho
Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Daniel Akuffo/Abdallah Juma dk64, Haruna Moshi
na Emanuel Okwi.
Azam FC; Deo
Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey
Morris, Abdulhalim Humud, Ibrahim Mwaipopo/Salum Abubakar dk 58, Himid
Mao, John Bocco, Abdi Kassim/Kipre Michael Balou dk 69 na Kipre Herman
Tchetche/Zahor Pazi dk 82.
![]() | |
| Kazimoto
katikati akiwapa salama mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao la
ushindi juzi. Kulia ni Juma Nyosso na kushoto Amir Abdallah Juma. Nyuma
ni Amri Kiemba. Chanzo:- Bin Zubeiry |


Post a Comment