Na.MO BLOG TEAM
Msajili
wa vyama vya siasa nchini Tanzania Bw. John Tendwa akisisitiza jambo
wakati wa mkutano na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake ambapo
amesema sasa ni mwanzo na mwisho kwa chama chochote cha siasa
kujihusisha na vurugu ambazo zinapelekea kutokea kwa mauaji. Hivyo
amewataka wanasiasa wote nchini kufanya siasa za busara bila vurugu ya
aina yoyote. Amesema hapendi mtu afe kwa ajili ya mikutano na kutaka
sasa tufikie mwisho wa mauaji.
Chanzo: Moblog

إرسال تعليق