Timu ya Queen Park Rangers siku ya Jumamosi ilizima
rekodi ya Chelsea ya kuzifunga timu tangu msimu wa ligi ya Uingereza
ianze mwaka huu baada ya kutoka sare bila kufungana bao lolote.
Kwa sare hiyo QPR ilijizolea pointi mmoja katika ligi hiyo.
Hatua ya mlinzi Anton Ferdinand
kukataa kumsalimia nahodha wa Chelsea John Terry kabla ya mechi kuanza
ilifanya mechi hiyo kukosa msisimko.
Beki huyo wa QPR pia alikataa kumsalimia mlinzi wa Chelsea Ashley Cole .

Anton alikataa kumsalimia Terry kutokana na
madai kwamba katika mechi yao ya msimu uliopita nahodha huyo wa Chelsea
alimkejeli na kumtolea maneno ya ubaguzi wa rangi.

Wakati wa Kesi hiyo Cole alikuwa shahidi upande wa Terry.
Lakini mahakama ya Uingereza ilimpata Terry bila ya makosa wakati alipofunguliwa mashitaka.
Hata hivyo katika mechi hiyo ya Jumamosi,Chelsea
walilalamika kuwa muamuzi aliwanyima nafasi za wazi mbili za kufunga
kwa njia ya penalti.

إرسال تعليق