![]() |
| TOTO AFRIKAN |
![]() |
| JKT OLOJORO |
![]() |
| BENCHI JKT OLOJORO |
![]() |
| BENCHI TOTO AFRIKAN |
![]() |
| GOLI ALILOKOSA MCHEZAJI EMMANUEL SWITA DAKIKA YA TATU YA MCHEZO. |
Timu
ya Timu kutoka Afrikan ya Mwanza leo imetoka sare ya goli moja moja
na timu ya JKT Olojoro katika mechi ya ufunguzi wa pazia ya ligi kuu
Tanzania Bara iliyochezwa leo katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Mechi
hiyo iliyokuwa na ushindani mkali kutoka pande zote mbili, Toto
walianza kwa kasi kwa kulisakama lango la JKT Olojoro na mnamo dakika ya
tatu Toto Afrikan walipata penalti ambapo mchezaji wake Emmanuel Swita
alikosa baada ya kipa ya JKT Olojoro Shaibu Issa kuipangua penalti hiyo.
Wachezaji
wa timu zote walicheza mchezo wa kuonana katika kipindi cha kwanza na
hadi mapumziko timu zote zilitoka bila bila na kwenda mapumziko.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Timu zote kushambuliana kwa hatamu na timu ya
Toto Afrikan wakipoteza magoli ya wazi kabisa. Kipa wa Toto Afrikan
alifanya kazi kubwa ya kuondoa michomo kibao kwenye lango la timu ya
Toto Afrikan.
Dakika
ya 88 timu ya Jkt Oljoro walipata goli la kwanza kupitia Hemedy Amri na
kisha Toto Afrikan kusawazisha dakika 89 kupitia kwa Mohamed Notto. Na
hadi mwisho wa mechi Toto afrikan moja na Jkt Olojoro moja.
Bplus blog





إرسال تعليق