 |
| Mjengo wenyewe nd'o huu |
 |
| Mchungaji Lwakatare akizungumza siku akiuzindua. |
 |
| Samani za ndani ya mjengo |
 |
| Kitanda ndani ya mjengo |
 |
| Mc akiwa kazini siku ya uzinduzi wa mjengo huo... hapa ni sehemu mojawapo ndani ya mjengo |
 |
| Hapa mchungaji akipozi kwa picha na Mc siku ya uzinduzi wa mjengo. |
 |
| Mc na mwenzake wakiwa kwenye kochi ndani ya mjengo huo. |
 |
| Kujisevia misosi siku ya uzinduzi wa mjengo. |
Lile 'jumba' kali la Mchungaji na Mbunge
wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Dk. Getrude Rwakatare na ambalo
lilidaiwa kuzinduliwa kwa mbwembwe hivi karibuni, ni miongoni mwa
majumba ya kifahari yanayotakiwa kuvunjwa mara moja kwa madai kwamba
yamejengwa kinyume cha sheria za mazingira kwani yote yapo katika maeneo
ya kandoni mwa mito ya Mbezi Beach, Mndumbwe na eneo la Hifadhi ya
Mikoko jijini Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa salama pekee ya
mjengo wa Mama Lwakatare unaokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. bilioni
1.5 itategemea maamuzi ya mahakama ambayo hadi sasa ndiyo iliyositisha
zoezi la kulivunja.
Jana, Mwanasheria wa Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche, alikaririwa
katika taarifa ya gazeti la NIPASHE akithibitisha kuwapo kesi
iliyofunguliwa na mmiliki wa jumba hilo katika Mahakama Kuu, Kitengo cha
Ardhi na kwamba itatajwa wiki ijayo (Septemba 20, 2012).
Baadhi ya majumba katika maeneo hayo
yameshabomolewa katika operesheni ambayo pia ilihusisha Wizara ya
Maliasili na Utalii na kusimamiwa na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
cha Jeshi la Polisi, Julai 7, mwaka huu, lakini jumba la Mama Lwakatare
liliachwa kutokana na kuwapo zuio la mahakama.
إرسال تعليق