Taasisi
ya Mawasiliano ya Afrika Mashariki (EACO) imefungua ofisi za
sekretarieti yake mjini Kigali, Rwanda ili kuratibu na kurahisisha
utendaji kazi wa taasisi hiyo.
Taasisi
hiyo iliichagua Rwanda kuwa makao yake makuu ya kudumu karibu miezi 14
iliyopita katika mkutano wake wa 18 uliofanyika mjini Kigali, Shirika
Huru la Habari la Afrika Mashariki linaripoti.
Kufuatia
uamuzi huo, ofisi hiyo iliyofunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita na
kuanza rasmi kazi zake ni inahusisha wajumbe wa bodi ya wakurugenzi tu.
EACO
ni taasisi ya kikanda inayoshughulika na udhibiti wa masuala ya posta,
mawasiliano na utangazaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Sekretarieti
hiyo itafanyakazi zake katika makao yake makuu ya muda yaliyomo ndani
ya ofisi za Taifa za Mamlaka ya Mawasilino nchini Rwanda zilizopo
katikati ya jiji la Kigali.
Lakini
mipango ipo mbioni ya kujenga ofisi zake za kudumu kwa ajili ya masuala
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ya taasisi hiyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya uzinduzi, Waziri wa Masuala ya EAC wa Rwanda,
Monique Mukaruliza alielezea uzinduzi huo kuwa ni hatua moja kubwa
katika mwenendo mzima wa kuleta mtangamano wa jumuiya hiyo.
‘’Kila
wakati tunapofanya vikao vya Baraza la Mawaziri huangalia itifaki
tulizotia saini, maamuzi tuliyotoa na hujiuliza sisi wenyewe ni
maendeleo gani tumeyafikia. Tuna uhakika kwamba wananchi wa Afrika
Mashariki wameanza kunufaika na mtangamano tunaouzungumzia? Huu ni mfano
hai kwamba wanaafrika Mashariki wanaweza kujipanga wenyewe na kufanya
jambo la maana,’’ alisema.
Waziri Mkaruliza ameahidi kutoa ushirikiano unaohitajika kwa EACO ili kufanikisha malengo yake.
‘’Ndoto
yetu katika mtangamano ili kupata umoja, maendeleo na ushirikiano sasa
inaendelea kuwa ya kweli kupitia uzinduzi wa ofisi za sekretarieti ya
EACO,’’ alisema Salvatory Nizigiyimana, Mwenyekiti wa EACO.
Nizigiyimana
ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Burundi
(ARCT) alielezea matumaini yake kuwa taasisi hiyo itakuwa chachu ya
kuleta maendelea kwa kukuza mawasiliano katika kanda hiyo.
إرسال تعليق