
"Kiukweli
nimesikitishwa sana na taarifa za mwanadada huyu kujinadi kua
anamahusiano na mimi ya kimamapenzi na eti tunamipango mingi ikiwemo ya harusi ndani yake...
Nimejiskia vibaya sana Kwani taarifa azitoazo msichana huyo si za
kweli kabisa, Nilikutana nae Malindi akiwa kama mmoja ya Waandaaji wa
tamasha hilo nililokwenda kutumbuiza na mbali ya hayo pia alikua ni
mdogo wa Mwenyeji wangu wa Malindi, hivyo nilikua nikimchukulia kama
dada yangu kumbe mwenzangu alikua anamipango mingine...
Nahisi
Ukarimu wangu kwake na kuwa nae huru kama mmoja ya wenyeji wangu
umeniponza, badala yake anatumia picha tulizopiga nae kwa namana
nyingine....
Ukweli ni kwamba MWANADADA HUYO SINA MAHUSIANO NAE YA KIMAPENZI KABISA.... MPENZI WANGU NAAMINI KILA MTU ANAMJUA.....".....Diamond
إرسال تعليق