
Wakili
wa kujitegemea mkoani Arusha, akisoma taarifa ya wasifu wa baba yake
mzee Augustino Lissu Mughwai (86) wakati wa misa ya mazishi wa mzee huyo
ambaye pia ni mzazi wa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Tundu
Lissu.Mzee Augustino alifariki dunia septemba 16 mwaka huu.

Waziri wa nchi, sera, uratibu na bunge Mh. William Lukuvi akitoa salamu kwenye msiba wa baba yake na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kijijini Mahambe.

Mwenyekiti
wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akifuatilia misa ya
mazishi ya baba mzazi wa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
MzeeAugustino Lissu Mughwai aliyefariki dunia Septemba 16 mwaka huu.

Waziri
wa nchi,sera,taratibu na bunge William Lukuvi (wa tatu kutoka kushoto)
akiwa kwenye msiba wa mzee Augustino Lissu Mughwai baba mzazi wa mbunge
wa jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu.Wa kwanza kushoto ni naibu
waziri wa maliasili na utalii,Lazaro Nyalandu na wa pili kushoto ni mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone.Wa kwanza kulia ni mbunge wa Karatu
CHADEMA,Israel Natse.

Wakili wa kujitegema mkoani Arusha, Allute Mughwai (wa
kwanza kulia) akifuatilia kwa makini misa ya mazishi ya baba yake mzee
Augustino Lissu Mughwai. Wa nne kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la
Singida mashariki,Tundu Lissu.

Mbunge
wa jimbo la Kigoma kaskazini Kabwe Zitto (kulia) akizungumza na mkuu wa
wilaya ya Ikungi Manju Msambya wakiwa kwenye mazishi ya baba wa mbunge
wa jimbo la Singida mashariki,Tundu Lissu.(Picha zote na Nathaniel
Limu).
إرسال تعليق