DAR ES SALAAM, Tanzania
Kundi zima la TMK Wanaume likionyesha staili yao ya Mapanga Shaaa jukwaani. (PICHA ZOTE/HABARI: ERICK EVARIST NA MUSA MATEJA/GPL).
SHINDANO
la kumtafuta Mfalme wa Mic (The Mic King), jana liliendelea katika
Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem na kuwapata wawakilishi 12 wa
wilaya ya Ilala huku burudani ya kufa mtu ikiporomoshwa na kundi la
Wanaume TMK na Bendi ya Extra Bongo.
Washiriki 12 waliopenya katika shindano hilo wakiwakilisha wilaya ya Ilala.
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (kulia) akiwa na wanenguaji wake jukwaani.
Memba mzee wa kundi hilo, Bibi Cheka (kushoto) akimwaga mistari jukwaani. Kulia ni Temba.
Mmoja wa washiriki wa The Mic King akionyesha uwezo wake jukwaani.
...The Mic King akiendelea kusakwa.
Majaji wa The Mic King, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ (kushoto), John Dilinga ‘DJ JD’, na Sister P wakifuatilia shindano hilo.
Mmoja wa washiriki akionyesha ufundi wa kurap.
Wanenguaji wa Extra Bongo wakionesha mambo jukwaani kuinogesha Dar Live.
Msanii anayesumbua na songi la Mwanayumba ndani ya gemu la Bongo Fleva, Chegge Chigunda, akimsaka ‘Mwanayumba wake’ jukwaani.
Zao jipya la Kundi la TMK Wanaume, mwanamuziki Getruda, akionyesha uwezo wake jukwaani.
(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST NA MUSA MATEJA/GPL)
إرسال تعليق