MIRIAM’ WA ‘BONGO MOVIE’ AGOMA KUOLEWA….NI BAADA YA WAZAZI KUCHUKUA MAHALI BILA RIDHAA YAKE



MSANII chipukizi kwenye tasnia ya filamu bongo, Miriam, ambaye ni mdogo wa msanii Jackine Wolper, amesema  kuwa yupo kwenye wakati mgumu kwani wazazi wake wanamtaka aolewe kilazima na
mtu ambaye hana mahusiano naye huku wakiwa tayari wameshachukua mahari.

Ishu hiyo awali kabisa ilidaiwa kuwa mwanaume ambaye amewekwa kwa ajili ya kumuoa ni mume wa mtu huku ndugu zake wakiwa wameshapokea nusu ya mahari tangu mwaka jana.

Mwandishi wa habari hizi, alimtafuta msanii huyo ili kuzungumza naye kwa kina juu ya hiyo, ndipo alipodai kuwa hawezi kusema lolote kwani haitaji kuolewa kwa sasa na kitu kikubwa kinachomtatiza ni kwamba mwanaume huyo tayari ni mume wa mtu.

Alidai baadhi ya ndugu zake wanadai kuwa nusu ya mahari imeshatolewa kwa ajili yake na endapo akikataa kufanya wanavyotaka hali itakuwa ngumu kwani hakuna kitu wanachoweza kurudisha kwa mwanaume huyo zaidi ya yeye kukubali kuolewa.

“Mimi siwezi kwa sababu sina mpango wa kuolewa kwa sasa lakini wazazi ndo kwanza wanataka mimi nifanye hivyo yani nashindwa kuelewa nifanye nini kwa hili, kila ndugu ninayemfuata kumbe anajua kila kitu juu ya hilo suala na walishindwa kunishirikisha mimi ili nitoe mawazo yangu,” alisema kwa unyonge.
credit kwa dartalk.com

Post a Comment

أحدث أقدم