Makamu
wa chuo cha VETA mkoani Singida,akizungumza muda mfupi kabla ya
kufunguliwa kwa mkutano wa madereva wa magari ya abiria mkoani Singida.
Kaimu
mkurugenzi mkuu wa SUMATRA Bw. Ahmad Kilima akizungumza kwenye hafla ya
kufungua mkutano wa madereva wa magari ya abiria mkoani Singida.Mkutano
huo uliofanikiwa ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha VETA
mjini Singida.Kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus
Sinzumwa.
Mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Singida, Mohammed Likwata
akitoa taarifa yake kwenye mkutano wa madereva wa magari ya abiria
ulioitishwa na SUMATRA.
Baadhi
ya madereva wa magari ya abiria waliohudhuria mkutano ulioitishwa kwa
ajili yao na SUMATRA.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Madereva
nchini wamehimizwa kuanzisha vyama vyao ili kujijengea mazingira mazuri
ya kuweza kukabiliana kisayansi na changamoto zinazowakabili ikiwemo ya
kulipwa maslahi duni na waajiri wao.
Wito
huo umetolewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa SUMATRA,Ahmad Kilima wakati
akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa madereva wa magari ya abiria
mkoani Singida.
Alitaja
changamoto zingine zinazowakabili madereva,kuwa ni kutokuwa na ajira za
uhakika na uwezo mdogo wa kujisomesha au kujiendelea kielimu,ili kuwa
na ufahamu mkubwa wa sheria na kanuni za usalama barabarani.
Kaimu
meneja huyo alisema SUMATRA inaamini kuwa wamiliki wa mabasi na malori
au waendeshaji wa makampuni ya mabasi na malori na madereva
wenyewe,kwa pamoja wanayo nafasi kubwa ya kuchangia kupunguza ajali
nchini.
إرسال تعليق