Na Khaleed Gwiji Zanzibar
Viongozi wa Uamsho wamepelekwa rumande baada ya Hakimu wa Mahakama ya
Wilaya iliyopo Mwanakwerekwe, Zanzibar, kuwanyima haki yao ya dhamana.
Ulinzi katika Mahakama hiyo na maeneo yaliyo pembezoni mwake ulikuwa ni mkali mno asubuhi ya leohadi kumaliza kwa shauri husika.
Washtakiwa walipandishwa kizimbani mnamo majira ya saa tano akiwemo: Sh.
Mselem, Sh. Farid, Sh. Azzan, Sh. Mussa, Sh. Suleiman, Sh. Khamis na
Nd. Hassan. Wote walisomewa shtaka lao baada ya kusomwa Hati ya Mashtaka
(Charge Sheet) na Wakili wa Serikali anaetoka Afisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka, Zanzibar ambayo pamoja na maelezo mengine, inaeleza shtaka
hilo kuwa ni: matamko ya uchochezi yaliyopelekea kufanyika kwa fujo na
uvunjifu wa amani yaliyotolewa tarehe 17, August, 2012, Magogoni,
Zanzibar.
Baada ya washtakiwa kusomewa shtaka na wote kulikataa, Wakili wa
Serikali aliiomba Mahakama kuipangia kesi tarehe nyengine kwa kuwa
upelelezi hakuwa umekamilika.
Unade wa Mawakili wa washtakiwa ukiongozwa na Mh. Abdallah Juma na
wenziwe wawili: Mh. Rajab na Mh. Suleiman kwa pamoja waliiomba Mahakama
mambo mawili:
Moja, wapatiwe Hati ya Mashtaka (Charge Sheet) ili kupitia kwayo wataweza kuwatetea wateja wao kwa ubora zaidi.
Pili, waliiomba Mahakama kuwapatia washtakiwa wote 7 dhamana zao sio tu
kwa kuzingatia kwamba dhamana ni haki ya washtakiwa ya Kikatiba; bali
pia kutokana na nature ya shtaka lenyewe la incitement to violence
ambalo ni kosa dogo (misdemeanour) na hivyo kulifanya kuwa ni bialable
offence.
Upande wa Mashtaka haukuwa na pingamizi kwa ombi hilo la kuwapatia
washtakiwa dhamana, ila Hakimu alisema kuwa kutokana na 'mazingira' ya
shauri husika, anazuia dhamana na hivyo washtakiwa wapelekwe rumande
hadi tarehe 25 ya mwezi huu ambayo ni Alkhamis.
Kilichoonekanwa na wengi ni simply incompetence and prone to fundamental
legal errors na jengine kubwa zaidi wengi wanaamini ya kwamba - an
unseen political hand clearly is a more plausible explanation.
Muhimu kwa sasa ni kuwa timu ya Mawakili wa washtakiwa inazidi kujipanga
kwa siku hiyo kuona kuwa washtakiwa wanapatiwa dhamana zao kama Katiba
inavyoidhamini haki hiyo lakini pia kama Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
Jinai iliyotumika kufungulia shtaka hilo nayo inavyoidhamini haki na
fursa hiyo kwa makosa yote nje ya makosa makubwa (felonies) kama mauaji,
uhaini nk.
Muhimu zaidi ni kuendelea kuitafutia Zanzibar yetu SOVEREIGNITY yake kwa
kupitia utaratibu wa amani, na demokrasia ambao msingi wake ni mawazo
ya walio wengi yanatawala.
Aidha, kudumisha Umoja wetu na kulinda Maridhiano ya Wazanzibari;
halikadhalika, kugombania maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari bila ya
kujali itikadi zetu za kisiasa, kabila, dini, jinsia au umri.
Kwa kuamini kwamba ni muhimu kuunganisha juhudi zetu: kuimarisha Umoja
wa Pamoja uliopo Zanzibar ikiwa ndio nyenzo muhimu ya kulifikia lengo
letu kwa njia za amani na utulivu la kuwa na Zanzibar yenye mamlaka na
madaraka kamili kitaifa na kimataifa na kufuatiwa na Mashirikiano ya
Kimkataba
إرسال تعليق