Kamishna
wa Polisi Zanzibar,Mussa Ali Mussa (pichani) aliwaambia waandishi wa
habari kwamba watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) walikamatwa sehemu
tofauti, mmoja amekamatwa Kisiwa kidogo cha Tumbatu, wa pili maeneo ya
Mjini Unguja,mtuhumiwa wa tatu alikamatwa ofisi za Idara ya Uhamiaji
alikokwenda kushughulikia hati ya kusafiria ili aweze kutoroka hapa
nchini.
Kamishna
Mussa alisema watuhumiwa wengine watatu wamekamatwa Mkoani Tanga ambako
walikimbilia kujificha baada ya kufanya mauaji ya Afisa Polisi Koplo
Said Abdulrahman.
“Watu
hao walitorokea huko na tunaendelea kuwahoji…tunawashukuru wananchi kwa
ushirikiano wao mkubwa uliotuwezesha kufanikisha ukamataji
huo,tunavishukuru vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyo katika Shehia
mbalimbali kwa kuimarisha ulinzi wa maeneo yao katika kipindi chote cha
fujo na vurugu hizo” Alisema Kamishna Mussa.
Kamishna
Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa Polisi hivi sasa inaendelea
kuwahoji Sheikh Farid Hadi na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Uamsho na
Mihadhara ya Kiislam ili kufahamu wapi alipokuwa na kuthibitisha kama
kweli alitekwa ama la.
Katika
hatua nyengine Polisi imeonya kuchukua hatua kali dhidi ya wafuasi wa
UAMSHO wanaodaiwa kutaka kuvamia kambi za Polisi,kambi za Majeshi na
Ofisi za Serikali ya Mapinduzi.
“Natoa
onyo kali kwa wananchi wote kuwa hakuna mtu yeyote aliye juu ya
sheria,Jeshi la Polisi na Vikosi vyote vya ulinzi na usalama tumejipanga
madhubuti kukabiliana na mtu yoyote ama kikundi chochote kitakachofanya
vurugu” Alisema Kamishna Mussa.
Akizungumzia
hali ya amani, Kamishna Polisi alisema kwamba Mji wa Zanzibar ni shwari
kwa sasa na wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
“Jeshi
la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha ulinzi,tunaomba
wananchi wasiwe na hofu na waendelee kutii sheria za nchi bila
kushurutishwa,waendelee kudumisha amani katika maeneo yao na pia
waendelee kutupatia taarifa za mara kwa mara za hali ilivyo huko
wanakoishi”
Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzibar
20/10/2012
إرسال تعليق