Anglikana Yateua Askofu Wa Kwanza Mwanamke

ELLINAH Wamukoya ameteuliwa kuwa Askofu wa Kwanza wa Kike wa Kanisa la Kianglikana barani Afrika. Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo ni heshima kwa kina mama. Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa kanisa hilo katika ufakme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata siasa za kihafidina. Kutawazwa kwake kumejiri huku Kanisa la Kianglikana, likitarajiwa kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa kanisa la Kianglikana barani Afrika.
Askofu wa jimbo la Capte Town, nchini Afrika Kusini, amesema kuwa wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili kujadilia sauala hilo kwa haraka. Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyombo vya habari, askofu huyo wa Jimbo la Cape Town, Revd. Thabo Makgoba, amesema wimbi kwa sasa linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao ni sawa na bingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na kukariri kuwa nia yao kuwa ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu mweusi, muafrika na raia wa Swaziland. Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa Mji Mkuu wa Swaziland Manzini.

-BBC/SWAHILI.

Post a Comment

Previous Post Next Post