 |
Nimefurahi
sana kuungana tena na Fernando Torres...! Rafael Benitez akionyesha
jezi yake katika klabu ya Chelsea baada ya kutambulishwa mbele ya
waandishi wa habari leo Novemba 22, 2012. |
 |
Benitez akipelekwa kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu yake mpya ya Chelsea leo. |
 |
Benitez akitua Chelsea |
 |
Sijui
nitafikisha mechi 10? Anyway... hapa nimefuata mkwanja tu ...! hapa
tayari keshatupia nguo za kazi na kuanza kazi ya kuifundisha Chelsea kwa
mara ya kwanza leo Novemba 22, 2012. |
 |
Nahodha John Terry wa Chelsea akielekea mazoezini na mkoko wake wa bei mbaya leo |
 |
Fernando Torres wa Chelsea akielekea mazoezini leo Novemba 22, 2012. |
 |
Hayaaa...! Anzeni kujifua sasa niwaone |
 |
Benitez akitoa maelekezo muhimu kwa straika Fernando Torres na mwenzake wakati wa mazoezi yao leo Nov. 22, 2012. |
 |
Sasa
nitatisha tena kama nilivyokuwa Liverpool....! Torres akikokota mpira
mbele ya kocha wake Rafael Benitez wakati wakiwa kwenye mazoezi yao leo
Novemba 22, 2012. |
 |
Hatukutaki...!
Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wakiandamana kupinga ujio wa kocha
Rafael Benitez katika klabu yao leo Nov.22, 2012. |
 |
Rafa nje...! Shabiki mmoja wa Chelsea akionyesha bango lake kupinga kuajriwa kwa Rafael Benitez |
LONDON, England
Kocha wa muda wa
Chelsea, Rafael Benitez amesisitiza kwamba hajaajiriwa na mmiliki wa
Chelsea, Roman Abramovich kwa sababu tu ya kufufua kiwango cha straika
Fernando Torres na amedai kwamba Mhispania huyo aliyenunuliwa kwa paundi
za England milioni 50 (Sh. bilioni 130) yuko 'fiti' kurejesha tena
makali yake akiwa Stamford Bridge.
Torres anamsifu Benitez kwa
kumfanya awe mmoja wa mastraika bora duniani wakati wa kipindi chake cha
kuwa kwenye kiwango cha juu kwenye klabu ya Liverpool na kocha huyo
aliyemrithi tRoberto Di Matteo katika klabu ya Chelsea ianaamini kuwa
kukutana tena kwa wawili hao kunaweza kuleta mafanikio kama ilivyokuwa
Anfield.
"Nilijua kila mmoja atazungumza kuhusu," alisema Benitez
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi uliofurika
kuliko kawaida.
"Kila mmoja anazungumzia kuhusu yeye (Torres)
kutofanya vizuri akiwa Chelsea, lakini wakati nilipoangalia mechi, mara
zote niliamini kwamba amekuwa katika mwelekeo mzuri sana. Kwenye mazoezi
leo, alionyesha kuwa katika hali nzuri na kwa pamoja, tunaweza kufanya
mambo makubwa kwa klabu hii.
"Hili si suala la Fernando tu.
Fernando ni mchezaji wa kiwango cha juu na ataimarika kama wengine.
Nitasema nimewaona wachezaji wengi mazoezini. Oscar, Ramires, (Cesar)
Azpilicueta, nawaona wakiwa katika hali nzuri sana.
"Tunaweza
kuwasaidia waimarike? Tutajiathidi kufanya kila tunachoweza. Najua ni
kwa namna gani wachezaji wote wanaweza kuwa wazuri. Fernando ni mmoja wa
wachezaji muhimu katika timu hii. Nitajitahidi kumuinua kiwango chake
kama nitakavyowainua wengine wote."
إرسال تعليق