 
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi 
na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wageni waalikwa 
wakati wa uzinduzi wa mpango kabambe wa Teknohama katika Sekta ya Elimu 
nchini uliofadhiliwa na Kampuni ya HUAWEI kutoka China leo.
Katika Mradi huo wa Teknohama 
itayowezesha Watanzania mbalimbali kutoka shule za Sekondari na Vyuoni 
kupata vifaa na mafunzo ya Sayansi na Teknolojia ili kusukuma mbele 
maendeleo katika nyanja za Uchumi na Kijamii.
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni 
ya HUAWEI kutoka China Bw. Bruce Zhang akizungumza katika hafla hiyo 
kwamba Mpango huu unaoitwa "Huawei ICT Star" itasaidia katika shule za 
Primary na Sekondari katika kusukuma mbele maendeleo ya Sayansi na 
Teknolojia nchini Tanzania.
Alisema katika Program hii 
itasaidia kuboresha miundo mbinu katika Sanyansi na Teknolojia ili kutoa
 mwamko kwa vijana wa Kitanzania kujifunza masomo ya Sayansi na 
Teknolojia.
 
 Balozi wa China nchini Tanzania
 Mh. LU YOUQING akitoa maelezo yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa 
Teknohama katika shule na vyuo nchini Tanzania.
Balozi alisema mpango huu ni 
mwendelezo wa uhusiano mwema kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa 
China katika nyanja mbalimbali za biashara uchumi na Kijamii.
Aliongeza kwamba Serikali ya 
China itaendelea na mikakati yake ya kusaidia nchi ya Tanzania ili 
kuweza kufikia malengo ya Milenia ya 2015.

Meza Kuu.
 
 Mgeni rasmi Mh. Mbarawa na Balozi wa China wakizindua rasmi mpango wa "HUAWEI ICT STAR" nchini Tanzania.
 
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi 
na Teknolojia Profesa Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Bw. Bruce
 Zhang wakitiliana saini kitabu cha makubaliano rasmi ya Ushirikiano 
katika Sekta ya Sayansi na Teknolojia kupitia Elimu.
 
Profesa Mbarawa akimkabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI.

Pichani Juu na Chini ni wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.

 
Mgeni rasmi Waziri Mbarawa akiondoka ukumbi baada ya uzinduzi
! ~~ Huawei Ascend Mate 7 Online Shopping ~~ !
ReplyDeleteHuawei Ascend Mate 7 Price In Dubai | Huawei Ascend Mate 7 Price In Uae
Post a Comment