
Kala Jeremiah
Rapper Kala Jeremiah ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake Dear God
ametoa nafasi moja kwa mashabiki wake kufanya remix ya wimbo wake huo
baada ya kukunwa na uwezo wao wa kucomment kwa vina kila siku
anapoweka status ukurasa wake wa Facebook.
Katika maelezo yake ambayo ametutumia, Kala anasema mashabiki wake
wamekuwa wakimtumia mistari ambayo hata yeye mwenyewe ameshangazwa na
uwezo wao mkubwa sana.
“SIKU HIZI KILA SIKU NIKIPOST KITU CHOCHOTE KWENYE PAGE YANGU YA FB,
MASHABIKI WANGU WANACOMENT KWA VINA. TENA KWA VINA VINGINE KAMA AMBAVYO
MIMI NIMEMALIZIA KWENYE WIMBO WA DEAR GOD. CHA KUFURAHISHA ZAIDI
WANATOA MISTARI AMBAYO HATA MIMI MWENYEWE NASTAAJABU YANI MISTARI
MIKALI MPAKA NATAMANI NINGEIPATA MIMI WAKATI NAUTUNGA ULE WIMBO’’
Baada ya kugundua kuwa wana vipaji ameamua kufanya remix ya ngoma
yake hiyo lakini anasema itakuwa remix tofauti sana na haijawahi kutokea
duniani kote.
“Tunaitaji wanawake 10 na wanaume 10 kuchana kwenye hii remix na
utaratibu utakao tumika kuwapata hao watu 20 utakuwa kama ufuatavyo
Jumatano hii tutaweka namba za simu kwenye page yangu ya facebook watu
ambao watataka kushiriki watapiga na kujitambulisha majina yao namba
za simu na kisha kuchana mistari yake atayotaka iingie kwenye remix hii
na wakati anachana tutakuwa tunarecord moja kwa moja baada ya hapo
tutaipitia mmoja baada ya mwingine ili kuchukua aliyefanya vizuri,”
yanasema maelezo yake.
“Wale waliofanya vizuri tutawapigia simu kwa namba ambazo watakuwa
wamezitaja,ambao tutakuwa tumewachagua watapewa utaratibu wa kwenda
kurecord ndani ya studio za Smart Music zilizopo Tabata Barakuda.
Ikumbukwe kila mtu atatakiwa kuchana mistari minne tu na ikumbukwe pia
huu wimbo hauta pigwa hewani ila utakuwepo kwenye album yangu
inayotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi ujao.”
إرسال تعليق