
Producer mkongwe nchini na God father wa Bongo Flava kama
anavyojulikana kwa sasa, P-Funk Majani yuko busy kuliko kawaida akiandaa
kile anachokiita No Name 12/12/12. Japo bado hajaweka wazi No Name
12/12/12 ni kitu gani hasa lakini inavyoonekana ni compilation albam ya
Bongo Records ambayo huenda ikatoka December 12 mwaka huu.
Katika kuikamilisha, Majani amekusanya maproducer kibao ambao wamechangia beat zao huku Master pekee ndiye aliyebakia.
“Brah! Everybody has made a beat 4 No Name except u!!
Dully,Dunga,ludigo,Akil the Brain,lamar,John Mahundi,Majani,Ema wa THT,”
ametweet Majani.
Naye Master J amejibu, “ Im on it bra, call u in a few days, cheers,”
na mwisho Majani kumalizia kwa kutweet,“thats wat the No Name team
wants to hear from the legend. Cheers Brah!
Huenda hivi karibuni Majani ataitangaza pia orodha ya wasanii watakaosikika kwenye No Name 12/12/12!!
إرسال تعليق