“NACHUKIZWA NA WASANII WABABAISHAJI KWENYE KAZI” – IRENE PAUL

Msanii Irene Paul (kulia) akiwa na mwandishi wa script mahiri Ally Yakuti.

MSANII wa tasnia ya filamu bongo Irene Paul, amefunguka kwa kudai kuwa upole wake haumfanyi aonekane mwenye nidhamu ya uonga, bali mara nyingine ni mkimya lakini huwa anachukizwa sana na wasanii wababaishaji ambao hawako makini na kile wanachokifanya.

Msanii huyo ameshashiriki kwenye filamu nyingi ikiwemo ‘Love Me Or Love Me Not’, ambayo ameshirikishwa na Rose Ndauka na uwezo mkubwa aliouonesha katika kazi hiyo ni wazi kwamba baada ya mwaka mmoja atakuwa ni miongoni mwa wasanii mahiri Tanzania.



Irene Paul alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakimuonea kwa sababu ya upole wake lakini mara zote huwa makini kwenye kazi na ndiyo maana filamu anayoshiriki anapenda kufanya kweli ili mashabiki wake waone nini anachokifanya hata kama ni mpole.

“Napenda kuwa mkweli pale ninapoona mtu kanifanya kitu kibaya ili aweze kujirekebisha lakini wengine wanapoona nakaa kimya basi wanajua kwamba nawaogopa kwa madai nina nidhamu ya uoga hapana, lakini kuna muda huwa napenda sana kuwa kama mjinga kuepusha malumbano,”alisema.

“Wasanii wengi wa kibongo suala la muda wameliweka nyuma sana na ndiyo maana unakuta filamu ilitakiwa kutoka wakati fulani haitoki kwa sababu wao wanafanya bila kufuata kalenda na mwisho wa siku unakuta watu wanachoka kuendelea kukaa kambini kwa sababu ya kujivutavuta kwa mtu mmoja,” aliongeza

Post a Comment

أحدث أقدم