
NEW DELHI, India
MWIGGIZAJI wa filamu wa nchini hapa, Saif Ali Khan ametangaza
kuingia mzigoni upya kumalizia kazi yake inayokwenda kwa jina la Race 2.
Uamuzi huo wa kuingia mzigoni kwa mwigizaji huyo kuna
maanisha kwamba ameamua kumuacha mkewe, Kareena Kapoor akiendelea kuwa katika
fungate na yeye kuendelea na kazi zake za uigizaji.
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Saif zinaeleza kwamba
mwigizaji huyo hakuwa na muda wa kusubiri zaidi ila amewaambia kwamba sasa
anaingia kuimalizia kazi hiyo ambayo aliianza na kuisimamisha wakati alipokuwa
akijiandaa na sherehe hiyo
Post a Comment