Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Na Zitto Kabwe
GAZETI la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL.

Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo
inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha
binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito
ya IPTL.
Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa
na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya
Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za
ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato
mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic
audit).
Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali
Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa
IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati
ya Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii.
Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu
January Makamba ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu
suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni
mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John
Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011
alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote
hizo hazikuzaa matunda.
Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi.

Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta
ya kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu
ndogo kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila
mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme,
Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina
cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni
asilimia 20 tu ya uwezo (installed capacity).
Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo
itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya
Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama
wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha
Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha
maji.
Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.

2. Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta
ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa
mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na
utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe
nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha
lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari
umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa
taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi
wa shilingi bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.
3. Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha
fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa
dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama
taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua
gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta
hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.
إرسال تعليق