“Yanga na Simba wamekuwa wazungumzaji wazuri kuhusiana na ujenzi wa viwanja, lakini hakuna kinachoonekana,” hayo
ni maneno ya Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo
katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Yassoda aliwataka kuiga mfano wa klabu changa kama
Azam FC ambao ndani ya muda mfupi wameweza kuwa na uwanja , alisema
wakati umefika kwa viongozi wa klabu za nchini kufata mfano wa klabu za
Ulaya.
Yassoda
aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza pato la klabu zao,
kuongeza ajira na kupeleka burudani karibu na wadau wao na kuwapa
burudani kwa sababu soka ni burudani pia

إرسال تعليق