Prof Ruth Meena akitoa elimu kwa wahariri juu ya mchakato wa katiba yenye kuangalia usawa wa kijinsia.
Washiriki wa warsha ya wahariri wa vyombo vya habari nchini
wameshauri katiba ijaya mbali ya kuwa usawa wa kijinsia pia katiba
kuweza kuwawajibisha wabunge ambao wamechaguliwa na kushindwa
kuwatetea wananchi wao bungeni na kuishia kusinzia.
Wakizungumza katika warsha maalum kwa wahariri wa vyombo vya habari
iliyoandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) leo katika ukumbi
wa Courtyard Hotel ,washiriki hao wamesema kuwa idadi kubwa ya
wabunge wamekuwa wakifika bungeni kwa ajili ya kupokea posho bila
ya kuwawakilisha wananchi na hata wanapopata nafasi ya kuuliza
maswali wamekuwa wakiuliza maswali ambayo hayawasaidii wananchi wao.
Hivyo walipendekeza kuwa ni vema katiba ijayo kuweza kuwabana
wabunge wa aina hiyo ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya wabunge
bungeni na kuwa na mbunge mmoja kwa kila mkoa tofauti na ilivyo sasa
kwa mkoa kuwa na wabunge zaidi ya watano.
Hata hivyo wametaka kuwa suala la usawa katika uongozi ni vema kuwepo
katika katiba mpya na suala la viti maalum kwa wanawake kuangaliwa
zaidi na ikiwezekana utaratibu huo wa viti maalum kwa wanawake
kufutwa kabisa.
Kwa upande wake mkufunzi wa warsha hiyo Prof.Ruth Meena alisema
kuwa ili kuwa na katiba nzuri ni lazima kuwepo kwa misingi imara
itakayosimamia katiba hiyo .
Kwani amsema kuwa kati ya mambo ambayo yamo katika katiba ya sasa na
wengi wanapenda kuingizwa katika katiba ijayo ila kilichofanya
kutofanya kazi vema ni usimamizi wa katiba kutokuwepo
|
Post a Comment