WABUNGE WASIO ULIZA MASWALI YA MAANA NA WANAOLALA BUNGENI WASICHAGULIWE

washiriki  wa warsha  hiyo
Prof Ruth Meena akitoa  elimu  kwa  wahariri juu ya mchakato  wa katiba yenye  kuangalia usawa wa  kijinsia.

Washiriki  wa  warsha ya  wahariri  wa  vyombo vya habari nchini  wameshauri katiba  ijaya mbali ya  kuwa usawa wa  kijinsia  pia  katiba  kuweza  kuwawajibisha   wabunge  ambao  wamechaguliwa na kushindwa  kuwatetea  wananchi  wao  bungeni na kuishia  kusinzia.

Wakizungumza katika warsha maalum kwa  wahariri  wa  vyombo vya habari iliyoandaliwa  na mtandao  wa jinsia Tanzania (TGNP) leo katika ukumbi  wa Courtyard Hotel ,washiriki hao  wamesema  kuwa idadi  kubwa ya  wabunge  wamekuwa  wakifika bungeni kwa ajili ya  kupokea  posho  bila  ya  kuwawakilisha  wananchi na hata  wanapopata nafasi ya  kuuliza maswali  wamekuwa wakiuliza maswali ambayo hayawasaidii wananchi  wao.


Hivyo  walipendekeza  kuwa ni vema katiba  ijayo  kuweza  kuwabana  wabunge  wa aina  hiyo ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya  wabunge  bungeni na kuwa na mbunge mmoja kwa  kila mkoa tofauti na ilivyo  sasa kwa mkoa  kuwa na  wabunge  zaidi ya watano.


Hata  hivyo wametaka  kuwa suala la usawa katika uongozi ni vema  kuwepo katika katiba mpya na suala la viti maalum kwa  wanawake kuangaliwa  zaidi na ikiwezekana utaratibu  huo  wa viti maalum kwa  wanawake  kufutwa  kabisa.


Kwa  upande  wake mkufunzi wa  warsha  hiyo Prof.Ruth Meena alisema  kuwa ili kuwa na katiba  nzuri ni lazima kuwepo kwa misingi imara  itakayosimamia katiba  hiyo .


Kwani amsema  kuwa kati ya mambo ambayo yamo katika katiba ya  sasa na wengi   wanapenda  kuingizwa katika katiba  ijayo ila kilichofanya kutofanya kazi  vema ni  usimamizi wa katiba  kutokuwepo

Post a Comment

أحدث أقدم