MKATA mayenu wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Grace Utete
‘Kiza Kinene’ juzikati alianza maandalizi ya kufunga mwaka vibaya baada
ya kupewa talaka mbili na mumewe aliyetambuliwa kwa jina moja la Abeid.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mapaparazi wetu, lilijiri mchana kweupe
katika Baa ya Ben Kinyaiya iliyopo Kinondoni, Dar huku mkurugenzi wa
bendi anayowajibika mnenguaji huyo, Asha Baraka na meneja wake, Khamis
Kayumbu ‘Amigolas’ wakishuhudia.
Baada ya mnenguaji huyo kupokea talaka, Ijumaa Wikienda lilimvaa na
kumuuliza kulikoni kupewa talaka baa, tena mbele ya viongozi wake ambapo
bila hata kupepesa macho alijibu kuwa haoni tatizo na kwamba
anaifurahia hali hiyo.
Hadi Ijumaa Wikienda linaondoka eneo la tukio, Asha Baraka alikuwa
amekaa kikao na aliyekuwa mume wa mnenguaji huyo lakini haikujulikana
kikao hicho kilihusu nini.

إرسال تعليق