OMOTOYOSSI NA WACHEZAJI WENGINE WA KIGENI WAFUKUZWA - ZAMALEK


Football | Egypt



Zamalek to let foreigners go



BEKI wa Zamalek ya Misri, Saied Yousef ametimkia Dhufar ya Oman kwa mkopo wa miezi sita, BIN ZUBEIRY imeipata hiyo kutoka superrsport.com.
Saied alijiunga na Zamalek msimu uliopita akitokea Al Masry ya Misri pia na aling'ara akiwa na White Knights.
"Tumekubali kumruhusu Saied aondoke, na itakuwa nzuri kwake na kwa klabu, ataendelea kulipwa na klabu” Alisema Mjumbe wa Bodi ya Zamalek, Ibrahim Yousef alipozungumza na supersport.com.
"Hajer ya KSA inamtaka beki wetu mwingine Hamada Tolba, lakini tumekataa ofa hiyo” alisema.
Yousef alisema Kocha Mkuu wa timu, Jorvan Vieira anataka kuwatema wachezaji wote wa kigeni kabla ya msimu ujao.
Zamalek ina wageni watatu, ambao ni Abdoulaye Cisse, Razak Omotoyossi na Alexis Enam.

Post a Comment

أحدث أقدم