Na Bosire Boniface, Garissa
Biashara imeanguka Garissa kufuatia wimbi la mashambulizi ya mauaji mwezi uliopita.
Hashim Ali Abdi, mfanyabiashara wa vipodozi mwenye umri wa miaka 43,
alisema kuwa Garissa imekuwa chaguo la wanunuzi madukani kutoka Jimbo la
Kaskazini Mashariki kwa muda mrefu sana, lakini mashambulizi ya hivi
karibuni yamewafukuza watu.
"Wateja wangu, hasa kutoka Wajir na Mandera, wanasema wanaogopa kuja
Garisaa kupata mahitaji yao," aliiambia Sabahi. "Ninawategemea wao kwa
kiwango kikubwa."
Mashambulizi yamekuwa yakiongezeka Garissa tangu mwezi uliopita.
Al-Shabaab wanahusishwa na shambulizi ambalo liliua maafisa wawili wa
polisi tarehe 16 Novemba na jengine lililoua askari watatu tarehe 19
Novemba, ambalo lilifuatiwa na ulipizaji kisasi ambao askari waliwapiga
wananchi na kuchoma moto biashara. Tarehe 11 Disemba, polisi iliatia
mbaroi watu sita huko Garissa ambao wametuhumiwa kupanga shambulio la
kigaidi.
Irene Muthoni, ambaye anamiliki Irene Delicacies Hotel, alisema wateja wamemkimbia kwa sababu ya mashambulizi.
"Wakati wa chakula cha mchana na usiku, hoteli ilikuwa inajaa watu,
lakini sasa wateja wamepungua sana," alisema, na kuongeza kuwa ikiwa
hali hii itaendelea mwezi huu wa Disemba hadi Januari, basi atalazimika
kufunga.
"Ninapoteza pesa," aliiambia Sabahi. "Kila mwezi, nilikuwa ninapata pesa
nyingi kuweza kulipia jengo na kuweka akiba kubwa, lakini sasa
ninalazimika kutumia akiba kwa kulipia kodi."
Zeinab Sheikh Mohammed, mkurugenzi wa Baraza la Biashara na Viwanda la
Kenya katika Jimbo la Kaskazini Mashariki, alisema licha ya vikwzo
hivyo, jamii ya wafanyabiashara ina matumaini kuwa hali itarejea kuwa ya
kawaida.
"Tunatarajia kuwa zaidi ya shilingi milioni 300 (dola milioni 3.5)
katika fursa za biashara zilipotea mwezi Novemba," aliiambia Sabahi, na
kuongeza kuwa baadhi ya biashara zilizochomwa moto na askari bado
hazijajirudi.
"Tumekuwa na mikutano mingi katika mabaraza ya mji pamoja na maafisa wa
usalama ili kutafuta mikakati ya kumaliza vurugu na kila mtu
nanawajibika," alisema. "Hakuna mtu aliye salama, kwa vile tulishuhudia
wananchi wakivumilia mashambulizi. Hilo linatupa suluhisho la kuimarisha
mashirikiano yetu [na polisi] ili kujenga mazingira yanayovutia kwa
biashara."
Ushirikiano wa wananchi ni muhimu kwa kushughulikia kwa usalama
Katibu wa Kamati ya usalama ya Garissa Hassan Shurie alisema ni muhimu
sana kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama ili kuwatambua
wahalifu katika jamii.
"Tulipoteza mwanachama mmoja wa kamati ya amani ambaye alipigwa risasi
na kuuawa pamoja na askari mmoja wa jeshi la Ulinzi la Kenya tarehe 9
Disemba, lakini tutaendelea kufanyakazi na maafisa wa usalama ili
kuwasafisha wahalifu," alisema.
"Wahalifu wanakusudia kujenga chuki za vikundi," alisema. "Mashambulizi
haya ni ushahidi kuwa hakuna aliye salama kwa hivyo tunatoa wito wa
mashirikiano ili kumaliza vurugu."
Mkuu wa Wilaya ya Garissa Mohamed Maalim alisema mambo yataimarika ikiwa kila mmoja anafanyakazi pamoja.
"Kila mtu ana mengi ya kufanya ili kuimarsha hali hii," aliiambia
Sabahi. "Vikosi vya usalama wamefanya wanavyoweza na kuhatarisha maisha
yao ili kurejesha amani lakini haliwezi kkufanya hivyo pekee."
Maalim aliwaomba wakazi kushirikiana na serikali katika usajili wa watu
unaoendelea ili kuisaidia serikali kusimamia mienendo ya wananchi, moja
ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa usalama uliofanyika katika
baraza la mji mwezi Oktoba.
"Usajili tayari umetayarishwa katika vitongoji vya Waberi, Iftin na
Galbet na wale ambao hawakujisajili watachukuliwa kuwa ni wahalifu,"
alisema.
Sheikh Abdullahi Salat, mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu la Kenya
huko Garissa, alisema kuwa mashambulizi yataimarisha tu maazimio ya
wananchi ili kuhakikisha amani.
"Ufunguo wa kushinda vita hivi ni kuungana pamoja na kufanyakazi kwa
karibu na vikosi vya usalama," aliiambia Sabahi. Badala yake, maafisa wa
usalama wana jukumu la kuendeleza imani ya wananchi ili kushinda vita
dhidi ya al-Shabaab, alisema.
Salat alisema kuwa fujo za tarehe 19 zilizofanywa na askari waliokuwa
wanapingwa kuuliwa kwa wenzao watatu, zimemomonyoa imani za wananchi.
Hata hivyo, alisema kuwa wakaz bado wanataka kushirikiana.
"Wakazi wameisaidia serikali kupambana na al-Shabaab kwa kujitolea kutoa habari na wataendelea kufanya hivyo," alisema.
Alisema adhabu ya pamoja kwa wakazi kutoka mikononi mwa vikosi vya
usalama haipaswi kurejea, na kwamba wanasubiri matokeo ya kamati ya
bunge ambayo inachunguza ghasia hizo.
Chanzo: sabahionline.com

إرسال تعليق