Kaimu
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya
kupokea msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa kutoka kwa wadau wa afya
wa Australia.

Muuguzi
mkuu wa Idara ya Afya kutoka serikali ya Australia Bi. Catherine
Stoddart (kushoto) akimkabidhi funguo za magari ya kubebea wagonjwa
Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli
katika viwanja vya wizara hiyo jijini Dar es salaam. Magari hayo 2
yaliyotolewa kwa msaada wa wadau wa afya wa mashirika yasiyo ya
kiserikali ya Austaralia yatapelekwa kusaidia utoaji wa huduma za afya
ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe.

Katibu
mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli(kulia)
akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) funguo za magari
mawili ya kubebea wagonjwa aliyokabidhiwa na wadau wa mashirika yasiyo
ya serikali kutoka Austaralia.

Wawakilishi
wa wadau wa afya mashirika yasiyo ya serikali kutoka Austaralia
wakiongozwa na Muuguzi mkuu kutoka Idara ya Afya ya serikali ya
Australia Magharibi Bi. Catherine Stoddart (wa pili kutoka kushoto
waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii mara baada ya kukabidhi msaada wa magari 2
ya kubebea wagonjwa.(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).

إرسال تعليق