
MPAKA
sasa tayari jumla ya wanamichezo 45, wamejitokeza kuchukua fomu za
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu.
Nafasi zinazowaniwa ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe wa Kamati ya
Utendaji kuwakilisha kanda 13 tofauti.
Waombaji
wapya 11 waliojitokeza leo (Januari 18 mwaka huu) ni Richard Rukambura
anayeomba urais wakati kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni
Kaliro Samson, Jumbe Magati, Richard Rukambura, Omari Walii, Ahmed
Mgoyi, John Kiteve, Stanley Lugenge, Francis Ndulane, Riziki Majara na
Hassan Othuman Hassanoo.
Mwisho
wa kuchukua fomu kwa waombaji wote ni leo (Januari 18 mwaka huu) saa 10
kamili alasiri. Fomu pia zinaweza kuchukuliwa katika tovuti ya TFF
ambayo niwww.tff.or.tz na kurejeshwa kupitia email ya tfftz@yahoo.com Pia Kanuni za Uchaguzi za TFF zinapatikana katika tovuti hiyo.
Orodha
kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo
na Richard Rukambura (Rais). Walioomba kuwania nafasi ya Makamu wa Rais
ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.
Kwa
upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Salum Chama na Kaliro Samson
(Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura,
Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra
Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly
Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo
(Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja
na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge
(Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein
Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey
Nyange, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majara na Twahili Njoki (Morogoro
na Pwani), Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na
Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari
Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
WATATU ZAIDI WAOMBA UONGOZI BODI YA LIGI KUU
Waombaji
watatu wapya wamejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa
Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22
mwaka huu.
Walioingia
leo (Januari 18 mwaka huu) kwenye kinyang’anyiro hicho ni Hamad Yahya
wa Kagera Sugar anayeomba uenyekiti wakati Christopher Peter wa Moro
United na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza wanaoomba ujumbe wa
Bodi kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza.
Orodha
kamili ya waombaji uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu ni Hamad Yahya wa Kagera
Sugar na Yusuf Manji wa Yanga wanaoomba uenyekiti wakati Makamu
Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.
Kwa upande wa wajumbe wawili kuwakilisha klabu za Daraja la Kwanza ni Christopher Peter Lunkombe wa Moro United ya Dar es Salaam na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza.
Post a Comment