![]() |
Tofauti na makocha
wengi wa Kizungu wanaokuja nchini kufanya kazi, katika mechi huwaachia
Wasaidizi wao wazalendo majukumu ya kuzungumza na wachezaji mchezo unapoendelea,
kocha wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig juzi katika mechi dhidi ya African Lyon
alikuwa akipigizana nao mwenyewe kelele, hadi kuna wakati mwamuzi wa akiba alisimama
kumuamuru aketi kidogo baada ya kusimama muda mrefu mfululizo akisema nao.
|
![]() |
Babu Liewig anasema nao |
![]() |
Babu anasema nao wakati wasaidizi wake wanakula kipupwe kwenye sofa |
![]() |
Hapa refa anakuja kumuambia akae |
![]() |
Hapa Julio aliinuka kumsaidia kusema nao |
![]() |
Refa anamuacha Julio asimame, anamuambia Babu akakae |
![]() |
Babu anauliza, mbona Julio humuambii akae, refa anamuambia huyu kasimama sasa hivi, we tangu maechi ianze bwana hadi sasa hivi mnaongoza 3-1 bado hujakaa tu |
![]() |
Babu kakubali yaishe anakaa |
إرسال تعليق