BABY MADAHA - "HUWA SIPENDI KUHUDHURIA MISIBA YA WATU MAANA NAOGOPA KUROGWA...!!!".


MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha  ametoa kali ya mwaka baada ya kueleza kuwa, mara nyingi hapendi kuhudhuria kwenye misiba kwa kuogopa kulogwa. 

Akiongea na mwandishi wa kipande hiki , msanii huyo alisema sehemu nyingi zenye mikusanyiko ya watu ndiko wale walozi wanakofanyia kazi yao ya kuwaloga watu ndiyo maana alikacha mazishi ya John Maganga, Mlopelo, Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Juma Kilowoko ‘Sajuki’.

“Yaani mimi siku hizi sipendi kabisa kwenda kwenye mikusanyiko ya wasanii na watu wengi kwani huko ndiko tunamalizana hivihivi kwa kulogana. Japo vifo vya wenzangu vimeniuma sana lakini sina la kufanya ila nawaombea kwa Mungu,”alisema Baby Madaha.

Post a Comment

Previous Post Next Post