Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika, Chipolopolo ya Zambia, leo
wamebanduliwa nje ya mashindano hayo baada ya kutoka sare 0-0 na Burkina Faso
katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
Burkina Faso ilianza mechi hiyo kwa bahati mbaya baada ya nyota wake Alain
Traore kupata jeraha na kuondolewa uwanjani baada ya dakika kumi pekee.
Traore amefunga magoli matatu zikiwemo mbili wakati wa mechi yao dhidi ya
Ethiopia ambayo walishinda kwa magoli manne ya yai.
Dakika chache baadaye Davis Nkausu, wa Zambia vile vile alijeruhiwa na
kuondolewa uwanjani na mahala pake kuchukuliwa na Joseph Musonda baadda ya
kugongana na mlinda lango wa Burkina Faso.
Kufikia wakati wa mapunziko timu hizo mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ya
kutofangana bao lolote.
Katika kipindi cha pili Zambia ilifanya mashambulio kadhaa katika lango la
Burkina Faso, lakini juhudi zao zligonga mwamba.
Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikigawamna alama moja kila moja
na hivyo Burkina Faso kusonga mbele baada ya kukusanya jumla ya alama tano nayo
zambia ikiridhika la alama mbili.
Nigeria imeongoza kundi hilo kwa jumla ya alama tano huku Ethiopia ikivuta
mkia na alama moja.
Kabla ya mechi hiyo Zambia ilikuwa na alama mbili na ilihitaji ushindi katika
mechi ya leo ili ifuzu kwa raundi iajyo sawa na Nigeria.
Hata hivyo mabingwa hao watetezi watajialaumu baada ya kukoso nafasi nyingi
za kufunga wakati wa mechi hiyo.
Collins Mbesuma na Rainford Kalaba hawakuonyesha mchezo mzuri kama
iliyotarajiwa na uamuzi wa kocha mkuu wa kumuacha nje nahodha wa Chipolopolo
huenda ukashutumiwa vikali, na mashabiki wa Zambia
إرسال تعليق