![]() |
Ingizo jipya la Uinted: Wilfried Zaha atajiunga na Manchester United majira ya kiangazi kwasasa ataendelea kutumiwa na Crystal Palace mpaka wakati huo. |
Manchester
United imefanikiwa kumnasa winga wa Cristal Palace Winfried Zaha kwa
ada ya uhamisho ya pauni milioni £15 wakati huu ambapo Ashley Young
akitazamiwa kukosekana katika mchezo wa michuano ya vilabu bingwa ulaya
dhidi ya Real Madrid kutokana na kusumbuliwa na mguu.
Young
alipatwa na maumivu hayo katika mchezo wa ligi dhidi ya Liverpool pale
United ilipochomoza na ushindi wa mabao 2-1 kufuatia kugongana na Daniel
Agger na inaarifiwa kuwa winga huyo amepatwa maumivu ambayo yatamuweka
nje kwa wiki nne.
Meneja
wa United Sir Alex Ferguson alitarajia kumtumia Young katika mchezo wa
ligi dhidi ya Tottenham wiki iliyopita lakini ikashindakana kutokana na
kwamba alitakiwa kufanyiwa uangalizi wa mguu wake na majibu yakimtaka
asubiri kwa wiki nne.

United
itatakiwa kutanguliza malipo ya awali ya pauni milioni £10 yakiwa ni
malipo makubwa kuwahi kutokea kwa mchezaji anayechezea timu inayoshiriki
ligi ndogo ya Championship ikiwa ni zaidi ukilanganisha wakati ambapo
Arsenal ilimchukua Theo Walcott kwa pauni milioni £6m wakati huo
akitokea Southampton mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 2006.

إرسال تعليق