Mwenyekiti
wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la kukusanya fedha kwa ajili
ya ununuzi wa vifaa vya ofisi zao Kulia ni msanii Mrisho Mpoto na Suzan
Lewis 'Natasha'.
WASANII wa muziki wa kizazi
kipya wakiwemo Harid Tunda ‘Tundaman’,
Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ na Vitalis Maembe wamejitosa kutoa burudani
katika tamasha la ‘Usiku wa Mastaa wa Filamu’ litakalofanyika keshokutwa kwenye
ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo lenye lengo la
kukusanya kiasi cha sh milioni 60 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi za
Shirikisho la filamu Tanzania (TAFF), limeandaliwa na TAFF kwa kushirikiana na
Vannedrick Tanzania Limited.
Mwenyekiti wa TAFF Simon
Mwakifambwa alisema maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo yamekamilika, hivyo
amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Alisema wameamua kusaka fedha
hizo ili kuweza kupatikana kwa vitendea kazi na fenicha ambazo zitaendana na
hali halisi ya sasa, pia kuwezesha watendaji wa shirikisho hilo.
Aliongeza kuwa, usiku huo
ambao utatawaliwa na burudani zaidi, mbali na wasanii hao wa bongo fleva, pia
wasanii wa filamu wanaoimba muziki wakiwemo Shilole, Hemed PHD, Masanja
Mkandamizaji, Bingwa wa Rivas Alex Macheje, Kitale, Snura na Jini Kabula.
“Pia tutakuwa na bendi ya
African Stars ‘Twanga Pepeta’Joti, The Super Star King Majuto
Shija, Mtunis, Rado, Dude, Mangi, Matata, Kingwendu na wengineo’,
alisema
Aidha, kutakuwa na shoo ya
sebene kutoka kwa kundi la Bongo Muvi Unity likiongozwa na JB, Ray, Irene
Uwoya, Jackline Wolper,Wema Sepetu, Steve Nyerere, Dk.Cheni, Mr.Chuz na Yobnesh
‘Batuli’ na wengine wengi.
Usiku huo ambao kiingilio ni
sh.7,000 , 15,000 kwa VIP na sh.2,000 kwa watoto umedhaminiwa na DTV, Global
Publishers, Lamada Hotel, Times Fm, Umoja Drink, Clouds Media na Vannedrick
Tanzania Limited.
إرسال تعليق