Jeshi
la Polisi linaonekana kufanya kazi zaidi kwa mazoea kuliko kuzingatia
mafunzo wanayopewa, pichani ni askari polisi aliyejeruhiwa na wenzake
baada ya kupigwa marungu kwa kutomjua kama nayeye ni askari hadi
alipopiga kelele ‘mtaniua mimi mwenzenu’ ndipo wakamuachia.
Kilichofuata
baada ya askari huyo kuachiliwa na wenzake alimalizia hasira zake zote
kwa wanafunzi hao kwa kutembeza kipigo (mkong’oto) mkali kwa wanafunzi
Chuo Cha IFM waliojaribu kutaka kulazimisha jeshi la polisi kufanya
mkutano mbele ya kituo cha Polisi Kigamboni badala ya kwenye viwanja vya
mpira eneo la Machava Kigamboni bila kujali kuwa wanafunzi hao walikuwa
wakikabiliana na moshi nzito wa mabomu ya machozi lakini pia walisha
kuwa chini ya ulinzi mkali na hakukuwa na sababu yeyote ya kuwapiga
hivyo.
Mbali
na askari huyo kulikuwepo na askari wengine wawili akiwemo mmoja wakike
naopia waliambulia kipigo hiko. Fuatilia picha za Askari huyo na
matukio aliyofanya .
Picha hii inakuonesha kwa karibu namna rungu lilivyompasua Askari huyu, hapa utapata picha kama huyu askari aliyepigwa kidogo tu baadaye akaachiwa ameumia hivi je wale waliopata mkong'oto wapo kwenye hali gani.
Hapa anazuia damu sehemu aliyopigwa isindelee kuvuja kwa kutumia kitambaa.
Baada ya kupata nafuu anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa kumkamata mmoja na kumpa kipigo cha nguvu hadi askari wenzake walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi huyo.
Hakuishia hapo aliwafuata pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na kumpa kipigo vile alivyojiskia ili amalizie hasira zake.
Kumbuka kipigo hicho kinafanyika mbele ya kituo cha polisi huku kukiwa na ulinzi mkali umeimarishwa.
Alichagua kama maembe au mpira na kuchezea alivyotaka!
إرسال تعليق