Mratibu wa Mpango wa kuboresha afya ya mama na mtoto, (JHI) wa Aga
Khan, Sisawo Konteh, akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa
afya ya mama na mtoto kwa Mkoa wa Morogoro. Mradi utakao wezesha upatikanaji
wa huduma bora za afya kwa mama na mtoto, Pamoja nae ( Katikati) Meya
wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo, na Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro
Elias Mtandu.
Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Elias Mtandu (Kushoto), akiwa
pamoja na Meya wa manispaa ya Morogoro Amir Nondo (Kulia) na Mratibu
wa mradi wa afya ya mama na mtoto wa Aga Khana Sisawo Konteh (Kushoto)
, wakinyanyua mikono ikiwa ni ishara ya kushikana mikono pamoja
katika kuunga mpango wa huduma bora ya Afya ya mama na Mtoto kwa Mkoa
wa Morogoro.
Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo akifungua Shampeni katika
uzinduzi wa Mpango wa Afya bora kwa Mama na mtoto kwa Mkoa wa morogoro.
Pamoja nae ni Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan Morogoro, Dr Hugo Yeste.
Mratibu wa mpango wa kuboresha afya ya Mama na mtoto ( JHI)
wa Aga Khan, Sisawo Konteh, akizungumza na Katibu tawala wa mkoa wa
Morogoro wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunga mkono huduma bora za
afya kwa mama na mtoto kwa mkoa wa morogoro
--
• Ni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii
• Mradi umefadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Kimataifa la Canada
• Hii ni kulingana na Malengo ya Maendeleo
ya Milenia 4 na 5
Morogoro, Januari 2, 2013 – Kituo cha Huduma za Afya cha AKHS kimezindua
mradi ambao utachangia kuboresha huduma ya afya ya mama mjamzito na mtoto nchini Tanzania
uzinduzi uliofanyika mkoani morogoro.
Mradi huo
unaojulikana kama Tushikane Mikono Kuboresha huduma kwa Wajawazito, na Afya ya
Mtoto (Joining Hands: Improving Maternal, Newborn and Child Health (JHI),
umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Canada (CIDA) kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania.
Mradi huo wa JHI
ni kulingana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs 4 na 5, ambao umelenga kuchangia
kuboresha uzazi kwa wajawazito na watoto wachanga, (MNCH) katika mikoa mitano ya
Tanzania.
Mradi huo
utatekelezwa kupitia Kituo cha Huduma ya Afya cha Aga Khan nchini Tanzania
(AKHST) na vituo vyake vitano vya afya ya awali (PMCs) kwenye mikoa ya Dodoma,
Mwanza, Mbeya, Iringa, na Morogoro ikiwa na lengo la kujenga uwezo wa huduma za
Afya kwa jamii na kuimaimarisha uhusiano na huduma ngazi ya rufaa.
Aidha, Mradio huo
wa JHI unajivunia Shirika la Kimataifa la CIDA juu ya uwekezaji mkubwa nchini
Tanzania na mtazamo wake juu ya nia yake ya kipaumbele kwenye sekta ya afya
nchini.
Mradi huo pia
utatumika kwa kuinua uwekezaji mkubwa uliofanywa na CIDA pamoja na serikali
katika kutekeleza mikakati yake.
Malengo ya mradi
huo wa JHI ni pamoja na: kuboresha ubora wa huduma kwa wajawazito, Afya ya
Mtoto na kulenga kuongeza uwezo wa maeneo ya mradi; kuongeza upatikanaji na
matumizi ya huduma za Wajawazito, Watoto na Afya ya Mtoto na kulenga watu wa
kipato cha chini na makundi ya wakazi maskini, na hasa katika kuongeza uwezo
wao wa kupata nafuu wa kupata huduma, ubora wa huduma za Afya ya uzazi na
Wajawazito, Watoto na huduma ya Afya kwa mtoto katika ngazi ya kwanza ya vituo
vya Afya; na kuboresha njia za afya, usafi na lishe ya familia kwa walengwa husika
(MNCH) kuongeza mahitaji ya huduma (MNCH) ubora kwa walengwa; na kuongeza
maarifa uhamisho na kubadilishana juu ya masuala muhimu katika Ushirikiano MNCH
Umma muktadha (PPP).
Mradi wa JHI wa
kuboresha Afya ya mama na mtoto
ulizinduliwa Julai 2012 nchini Tanzania na unatarajiwa kuendelea hadi mwaka
2015.
Mwisho …
Mhina Shabani.
Media Executive GDCC
0764 61 54 81
إرسال تعليق