Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akimkabidhi jezi ya timu hiyo, Paschal Ochieng wakati wa kumsajili |
Na Boniface Wambura
KAMATI ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka huu chini ya
Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imeliondoa shauri lililokuwa mbele yake dhidi ya
klabu ya Simba lililowasilishwa na wachezaji Pascal Ochieng na Daniel Akuffo
baada ya pande hizo kufikia makubaliano.
Wachezaji
hao kutoka Kenya na Uganda waliwasilisha malalamiko mbele ya kamati wakipinga
kukatizwa mikataba yao bila kulipwa stahili zao. Hata hivyo, pande zimefikia
makubaliano ya kuvunja mikataba nje ya kamati, na wachezaji hao kulipwa stahili
zao.
Aidha, Simba
imekiri kudaiwa na wachezaji Shija Mkina, Swalehe Kabali, Victor Costa na Rajab
Isiaka na kuahidi kuwalipa wachezaji hao wakati Coastal Union na mchezaji wake
Mohamed Issa wamefikia makubaliano ya malipo, hivyo kuvunja mkataba kati ya
pande hizo mbili.
إرسال تعليق