![]() |
Mbrazil Oscar akiisawazishia Chelsea bao la kwanza |
LONDON, ENGLAND
KOCHA
aliyepoteza mwelekeo Chelsea, Rafa Benitez amezidi kujipalia makaa ya
moto wakati vijana wake wakibanwa mbavu na kutoka sare ya mabao 2-2 na
timu ya Ligi Daraja la Pili, Brentford.
Katika
mechi hiyo ya raundi ya nne ya Kombe la FA, iliyopigwa Jumapili kwenye
dimba la Griffin Park, Chelsea iliokolewa na bao la Fernando Torres
dakika saba kabla filimbi ya mwisho.
Mchezaji
aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Fulham, Marcello 'Del Boy' Trotta aliipa
uongozi Brentford dakika mbili kabla mapumziko baada ya presha kubwa
kwenye ngome ya Chelsea ilioyoongozwa na John Terry.
Kipindi
cha pili, Chelsea ilikianza kwa nia ya kutaka kusawazisha, na Mbrazil
Oscar akafanikiwa kuweka mambo sawa dakika 10 baada ya kuanza kipindi
hicho.
Marcello Trotta akishangilia bao lake
Lakini Chelsea ilijikuta tena ikiwa nyuma baada ya Harry Forrester kuifungia bao la pili Brentford kwa mkwaju wa penalti.
Kuona
mambo yanakuwa magumu, Benitez aliwaingiza Cesar Azpilicueta, Juan Mata
na Demba Ba, lakini aliyemuokoa alikuwa Torres kwa kufunga bao la
kusawazisha dakika ya 83.

KIMYA! Torres baada ya kuisawazishia Chelsea bao la pili
Benitez alikutana na hasira za mashabiki wa Chelsea waliokuwa wakimzomea muda wote wa mchezo.
Timu hizo sasa zitalazimika kucheza mechi ya marudio kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mwezi ujao kusaka timu ya kusonga mbele.
Katika
matokeo mengine mabaya zaidi kwa vigogo vya Ligi Kuu ya Engaland katika
michuano hii ya FA ,ni ile ya Tottenham Spurs iliyochapwa na Leeds
United 2-1 na Liverpool ikiambulia kichapo cha 3-2 kutoka kwa Oldham
Athletic.
Kwa matokeo hayo Liverpool na Tottenham zimeaga rasmi michuano hiyo.
Post a Comment