KOMBE LA FA: SIKU MBAYA KWA VIGOGO …BENITEZ AJIPALIA MKAA CHELSEA IKIAMBULIA SARE, LIVEPOOL NA TOTTENHAM ZAFUNGASHA VIRAGO

OSCAR SEASON ... Chelsea ace levels
Mbrazil Oscar akiisawazishia Chelsea bao la kwanza
 
LONDON, ENGLAND

KOCHA aliyepoteza mwelekeo Chelsea, Rafa Benitez amezidi kujipalia makaa ya moto wakati vijana wake wakibanwa mbavu na kutoka sare ya mabao 2-2 na timu ya Ligi Daraja la Pili, Brentford.
Katika mechi hiyo ya raundi ya nne ya Kombe la FA, iliyopigwa Jumapili kwenye dimba la Griffin Park, Chelsea iliokolewa na bao la Fernando Torres dakika saba kabla filimbi ya mwisho.

Mchezaji aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Fulham, Marcello 'Del Boy' Trotta aliipa uongozi Brentford dakika mbili kabla mapumziko baada ya presha kubwa kwenye ngome ya Chelsea ilioyoongozwa na John Terry.
Kipindi cha pili, Chelsea ilikianza kwa nia ya kutaka kusawazisha, na Mbrazil Oscar akafanikiwa kuweka mambo sawa dakika 10 baada ya kuanza kipindi hicho.

Marcello Trotta celebrates
Marcello Trotta akishangilia bao lake
Lakini Chelsea ilijikuta tena ikiwa nyuma baada ya Harry Forrester kuifungia bao la pili Brentford kwa mkwaju wa penalti.
Kuona mambo yanakuwa magumu, Benitez aliwaingiza Cesar Azpilicueta, Juan Mata na Demba Ba, lakini aliyemuokoa alikuwa Torres kwa kufunga bao la kusawazisha dakika ya 83.

Fernando Torres celebrates his leveller
KIMYA! Torres baada ya kuisawazishia Chelsea bao la pili
Benitez alikutana na hasira za mashabiki wa Chelsea waliokuwa wakimzomea muda wote wa mchezo.
Timu hizo sasa zitalazimika kucheza mechi ya marudio kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mwezi ujao kusaka timu ya kusonga mbele.
Katika matokeo mengine mabaya zaidi kwa vigogo vya Ligi Kuu ya Engaland katika michuano hii ya FA ,ni ile ya Tottenham Spurs iliyochapwa na Leeds United 2-1 na Liverpool ikiambulia kichapo cha 3-2 kutoka kwa Oldham Athletic.

Luis Suarez nets Liverpool's leveller
Suarez akiifungia bao Liverpool
Kwa matokeo hayo Liverpool na Tottenham zimeaga rasmi michuano hiyo.

Post a Comment

أحدث أقدم