Pengine neno zuri la kumwambia Mario Balotelli
ni kila la kheri na unaweza pia kumpongeza kutokana na mengi
yaliyomkuta Manchester City lakini anapaswa kushukuriwa kwa kutuachia
kumbukumbu nzuri isiyosahaulika katika kipindi chote cha utumishi wake ndani ya viunga vya City of Manchester au Etihad stadium.
Baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka mitatu Manchester City hatimaye Mario Balotelli amerejea Italia katika klabu yake ya zamani ya AC Milan kwa mapango wa uhamisho wenye thamani ya pauni £20.
Sura mbalimbali za Balotelli ambaye ametokezea katika matukio mengi yaliyoibua gumzo na mara chache kicheko ndani ya Manchester City
Kueleka katika mchezo wa upinzani mkubwa katika soka la nchini ItaliaThe Milan derby anatazamiwa kuwepo kikosini katika timu yake hiyo dhidi ya Inter Milan mchezo ambao utapigwa jumapili ya 4 February.
Tukirudi ndani ya miaka yake mitatu ya soka ndani ya Manchester City, Balotelli amekuwa na mambo kadhaa ya yenye sura tofauti katika ligi kuu nchini England ikiwa ni pamoja na kipaji, kufunga magoli au kuwa msaada wa kupatikana magoli lakini usisahau matukio ya ghasia na ugmvi katika uwanja wa mazoezi upuuzi kadi nyekundu na hata kuvunja sheria nje ya uwanja.
Tukio la kurusha fataki akiwa bafuni katika nyumba aliyokuwa akiishi lilikuwa gumzo pia ndani ya kipindi cha miaka hiyo mitatu jijini Manchester ambalo hakika lilikuwa gumzo.
Mapema mwezi huu Balotelli alihusika katika tukio hasira na ghasia baina yake na meneja Roberto Mancini katika uwanja wa mazoezi.
Pia katika mchezo wa ushindi wa mabao 6-1 waliyopata City dhidi ya Manchester United mchezo wa ligi kuu ya England jambo ambalo liliibua gumzo kwa kijana huyu mwenye umri wa miaka 20 lilikuwa ni aina ya ushangiliaji wake ambao uliwavutia wengi wa 'look at me' na baadaye kuibuka na style nyingine ya kuonyesha fulana yake ya ndani ya jezi iliyokuwa na maandishi yanayosomeka Why always me, huyo ndio Mario Balotelli aliyekuwepo Manchester City.
Balotelli akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza katika dimba la Old Trafford October 2011
Balotelli
pia alihusika katika matukio ya ajali katika jiji la Manchester ikiwa
ni wiki chache baada ya kusaini City mwezi August 2010 kama gari yake
ilivyoonekana katika picha hapo juu.
إرسال تعليق